Please wait.....

Mwanzo Ingia Sajili Wasiliana

Save wild Hatifungani

ni mfumo ambao unamwezesha mwanachama kuwekeza katika shirika na baadae kurejeshewa fedha ikiwa na ongezeko la faida baada ya miezi 12 hadi 36.

Uzalishwaji wa faida

Fedha iliyowekezwa hutumika kununua mazao yaliyo rafiki kwa mazingira yanayozalishwa na jamii zinazoishi karibu na hifadhi za misitu na wanyamapori . Mazao haya ni pamoja na Asali, uyoga na Mpunga.

Mfano wa ongezeko la hatifungani

Mwanachama akinunua hatifungani ya Tsh. 10,000/= atatakiwa kulipia kila mwezi (Tsh. 10,000/=) katika kipindi cha miezi 12 hadi 36. Katika kipindi cha miezi 36 atakuwa amechangia jumla ya Tshs. 360,000/=. Fedha hii itarejeshwa ikiwa na ongezeko la asilimia 54% yaani Tshs. 554,370/=.
Bei ya hatifungani kwa kila mwezi Kiwango baada ya miezi 36(Tshs) Ongezeko la faida baada ya miezi 36 Ongezeko baada ya miezi 36
10,000 360,000 54% 554,370
20,000 720,000 54% 1,112,000
30,000 1,080,000 54% 1,668,000

Marejesho ya hatifungani

Mwanachama atatakiwa kuwasilisha nakala ya fomu aliyojaza wakati ananunua pamoja na viambatanishi muhimu ili aweze kupata marejesho yake. Marejesho yatafanyika ndani ya siku 14 baada ya mwanachama kuwasiliisha nakala ya fomu.

Maswali yanayoulizwa sana

Je endapo kutatokea hasara ktk biashara nini hatma ya marejesho pamoja na Faida?

Bodi ya wadhamini na menejimenti imejiridhisha kuwa uendeshaji wa mfomo huu kupitia mpango biashara wake utaleta faida kwa mwanachama na shirika hivyo itakuwa tayari kuwajibika endapo kutakuwa na tatizo lolote katika marejesho pamoja na faida.

Je mwanachama anaweza kusitisha hatifungani na kurejeshewa fadha yake?

Ndio, mwanachama ana uwezo wa kusitisha ununuzi na ulipaji wa hatifungani muda wowote endapo ataona mfumo huu hauna manufaa kwake. Kwa kulinda uhai wa mfumo, mwanachama atapewa faida pale tu hatifungani yake itakupofikisha muda wa kupevuka.

ECOWICE ni NGO, kwa nini inajihusisha na masuala ya kibiashara?

ECOWICE inatumia mfumo wa hatifungani kama njia ya kupata mtaji wa kununua mazao kutoka kwa wakulima kwa lengo la kuwawezesha kupata soko la uhakika. Pia ni njia mojawapo ya shirika kujiingizia mapato iliyoruhusiwa katika sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali ya mwaka 2002

Je, ECOWICE imejipangaje kupambana na ushindani ulioko katika sekta ya mazao inayopanga kuwekeza?

ECOWICE imefanya tafiti za masoko pamoja na changamoto za biashara ya mazao pia inatumia wataalamu na wazoefu wa kufanya biashara ya mazao.

Je, Unaweza kununua hatifungani zaid ya Tshs 30,000/=?

Ndio unaweza kununua hatifungani zaidi ya Tshs 30,000/=.